Government Job, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
WIMBI la wabunge kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM), liliendelea tena jana wakati Mbunge wa Siha, Dk. Godwin Mollel, alipotangaza kuhama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kujivua wadhifa wake. Katika taarifa yake iliyosambazwa pia kwa njia ya video, Mollel alikaririwa akisema ameamua kuhamia CCM baada ya kuridhishwa na utendaji wa serikali ya sasa ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.
Hatua hiyo ya Mollel ni mwendelezo wa uamuzi kama huo uliofanywa na wabunge wengine katika siku za hivi karibuni, akiwamo Maulid Mtulia aliyekuwa mwakilishi wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Wananchi (CUF).
Mtulia alijiondoa kwenye chama chake kilichomo katika Ukawa na kuhamia CCM baada ya kile alichoeleza kuwa ni kuvutiwa na utendaji wa serikali ya sasa.
Aidha, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM, Lazaro Nyalandu, alifanya uamuzi kama huo pia kwa kujivua ubunge na kuhamia Chadema akitokea CCM.
Akieleza zaidi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mollel alisema amechukua uamuzi huo kutokana na dhamira yake kumtuma kuwa anawajibu wa kushirikiana na viongozi wa nchi wakiongozwa na Rais Magufuli katika kupigania rasilimali za nchi.
“Dhamira yangu imeshindwa kuukataa ukweli huu kuwa hivi sasa uongozi wa nchi yetu chini ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), umedhihirisha wazi kupigania rasilimali za nchi… nimejikuta sina namna nyingine zaidi ya kujivua uanachama wa Chadema na kujiuzulu ubunge wangu ili niungane na CCM katika jukumu hili muhimu kwa taifa,” alisema Mollel katika taarifa yake na kuongeza:
“Huu ni uamuzi wangu mwenyewe, nimeufanya nikiwa na akili timamu na sijashinikizwa na mtu yeyote na nimefanya kwa sababu dhamira yangu inanituma kuwa nina wajibu wa kushirikiana na viongozi wa nchi wakiongozwa na Rais John Magufuli kupigania rasilimali za nchi,” alisema.
Akizungumzia uamuzi wa Mollel, Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), Anthony Komu, alisema kwanza hawaamini kama ni kweli, lakini kitendo hicho kinashangaza na kinatia wasiwasi kwa mustakabali wa siasa nchini.
“Nimeumia sana kwa kilichotokea. Lakini haya mambo ngoja tuone kama ni kweli. Bado mimi binafsi siamini Mollel amejiuzulu. Kama ndivyo kuna shaka katika siasa za Tanzania kwa sasa," alisema.
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) mkoa wa Kilimanjaro, Grace Kiwelu, alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu taarifa zinazoenea za kujiuzulu kwa mbunge huyo, alisema amezipokea kwa mshangao ingawa wao (Chadema) bado hawajapata taarifa rasmi.