Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa ameanza kuonyesha makali yake kwenye kikosi cha Tenerife B kwa kufunga mabao mawili na kutegeneza matano katika mechi 10 alizocheza.
Farid alikuwa akisumbuliwa na majeruhi ya muda mrefu yaliyomfanya akose mechi nane za mwanzo za ligi daraja la nne ‘Tercera’.
Kushiriki Tercera kwa kikosi B ni kwa lengo la kuwajenga wachezaji wanaochipukia kwenye kikosi hicho kiushindano kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza.
“Nimerudi kutoka majeruhi na nimeanza kucheza kwenye kikosi cha vijana, tupo nafasi 3 kwenye Tercera na pointi 37. Napambana kupata nafasi kikosi cha kwanza,” alisema Farid.
Tangu alipojiunga na Tenerife akitokea Azam mwaka jana Farid bado hajafanikiwa kupata namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Government Job, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
 
Top