2017 Government Job,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, Search for jobs in my area job postings,
NI wazi kitendo kilichofanywa na mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma cha kuikacha timu hiyo kwa kisingizio cha kuwa majeruhi kimelikera benchi la ufundi na sasa wamepanga kushusha washambuliaji watatu kwa ajili ya kuwafanyia majaribio ili wasajiliwe.
Yanga inayodhaminiwa na kampuni ya Sportpesa imepanga kuachana na Ngoma na sasa wanasaka mshambuliaji mwenye uwezo zaidi kwa ajili ya kuimarisha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo ambaye watamsajili kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili Desemba 15.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya usajili ya timu hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Hussein Nyika aliiambia Nipashe jana kuwa nyota hao kutoka katika nchi za Nigeria, Guinea na Sierra Leon wanatarajiwa kuwasili mapema wiki ijayo.
“Siyakumbuki majina yao, lakini wanakuja kufanya majaribio na kama benchi la ufundi litaridhika na mmoja wapo tutamsajili, kwa sasa hakuna namna ni lazima tusajili kwa sababu Ngoma (Donald) haeleweki na ni kama kaweka mgomo kuichezea Yanga,” alisema mjumbe huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Alisema kuwa usajili utakaofanywa katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili ni mapendekezo ya kocha George Lwandamina aliyoyatoa kwenye ripoti yake.
“Tumemsajili Mkomolwa (Yohana) ni mapendekezo ya kocha, lakini pia ametaka mshambuliaji mwingine wa kimataifa mwenye kiwango kikubwa,” aliongeza kusema Mjumbe huyo ambaye pia yumo kwenye Kamati ya Utendaji ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara.
Ngoma ambaye aliondoka hapa nchini kwa madai ya kwenda kujitibia Zimbabwe, yumo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Chalenji inayoanza kutimu vumbi keshokutwa nchini Kenya.Wachezaji wa Yanga wamepewa mapumziko ya wiki moja na wanatarajia kuanza mazoezi Jumanne kwenye uwanja wa Uhuru,
Chanzo: Nipashe