Tangazo la Kazi,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
KAMA ni shoo basi hii ndiyo ile inayoitwa ya kibabe. Si unajua Yanga inahaha kumpata straika mwenye misuli, akili na mashuti yenye hesabu za hadhi ya Ligi ya Mabingwa Afrika?
Basi bwana, kocha wa Wana Jangwani hao, George Lwandamina, analo jina la Mghana mwenye sifa hizo, Adam Ziriku, anayekipiga Nkana Rangers ya Zambia ambaye kama si kocha huyo Mzambia kutumia akili ya ziada, nusura jamaa angetimkia Afrika Kusini.
Wakati Yanga ikijiaminisha kuwa itampata straika huyo kwa wepesi, Baroka FC ya Sauzi kumbe imetuma watu wake kumtazama nyota huyo, lakini Lwandamina amefanya kazi moja kubwa ya kuhakikisha Mghana huyo hawaponyoki kirahisi kwani yupo kwenye mipango yake.
Kilichowavutia Baroka inayoongoza Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) ni ufanisi wa mshambuliaji huyo aliyefunga mabao 12 katika mechi 11 ndani ya Rangers na leo Jumamosi anacheza mchezo wa kuhitimisha Ligi Kuu Zambia.
Licha ya Baroka kuonekana kuwa na nguvu kubwa kifedha kuliko Yanga, lakini Lwandamina ametumia ukaribu wake na wakala wa mchezaji huyo, Joseph Mwalla, kurahisisha kazi ya nyota huyo kutua Jangwani.
Akizungumza na Mwanaspoti Mwalla amekiri kama isingekuwa mawasiliano ya mara kwa mara kati yake na Lwandamina yaliyoiweka Yanga katika hatua za mwisho za kumpandisha ndege Zikiru kuja Bongo, basi Baroka ingemchukua.
Yanga tayari imeanza mchakato wa kuhakikisha nyota huyo anatua nchini mapema wiki ijayo, jambo ambalo limerahisisha kazi ya kumleta klabuni hapo.
Lwandamina amekuwa na wasiwasi juu ya uwezekano wa mastraika wake, Donald Ngoma na Amissi Tambwe kurejea uwanjani kwa wakati, hivyo kupendekeza kwa mabosi wake usajili wa nyota wengine wa maana.
Ngoma ndiye amewekewa mstari mwekundu kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu, lakini Tambwe pia anatazamwa kama atakuwa fiti mapema.
Mwalla alisema straika wake huyo anaweza kuisaidia Yanga na bahati ni kwamba walishafanya taratibu za kumleta nchini mapema zaidi.
“Hao Yanga wana bahati kwani wanamtaka Zikiru kwa majaribio, lakini Baroka ilishatuma watu hapa Zambia tangu jana (juzi Alhamisi) na kesho (leo Jumamosi) watakuwa uwanjani hapa Zambia kwenye mechi ya mwisho ya ligi,” alisema Mwalla.
“Yanga walichofanikiwa ni kumaliza kila kitu katika safari ya Adam, lakini pia namuheshimu sana Lwandamina.”
Yanga inamtaka Zikiru kwa majaribio ili kumtazama sambamba na mastraika wengine, Mguinea Bensua Da Silva na Msierra Leone Badara Kella watakaotua mapema wiki ijayo.
Kama mastraika wawili watamvutia Lwandamina, huenda wakasajiliwa wote na Tambwe na Ngoma wakakatwa kwa pamoja.
Chanzo: MwanaSpoti
nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
 
Top