Tangazo la Kazi,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, ameibukia Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), huku akiwataka kutii uamuzi uliofanywa na vikao vya juu vya chama katika uchujaji wa majina ya wagombea

Sambamba na hilo, Pinda amewataka vijana kuchagua mtu ambaye anachukia makundi na ni mwadilifu na kutochagua wagombea wanaotoa rushwa na wenye makando kando.
Pinda alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua Mkutano wa UVCCM Mkoa wa Dodoma ambao ni kwa ajili ya uchaguzi wa nafasi mbalimbali za viongozi ikiwamo ya Mwenyekiti wa umoja huo.
Alisema chama kimeweka utaratibu wake, hivyo hakuna sababu ya uchaguzi kushindwa kufanyika au kuendeshwa vibaya kwa kuwa kila jambo limeandaliwa, kinachohitajika ni utekelezaji.
“Kuna wakati huwa najisikia faraja sana kuwa ndani ya CCM kwa kuwa ni chama ambacho nimelelewa nacho nimekuwa nacho, lakini kila wakati najiuliza wapi tena chama kizuri kama hiki ambacho kinatekeleza demokrasia kuanzia kwenye shina, tawi, kata, wilaya, mkoa na taifa?” Alisema.
Alisema mfumo uliopo kwenye chama ndio upo kwenye jumuiya zake ikiwa ni pamoja na UVCCM ambako wana fursa ya kipekee ya kutoa uhai wa chama.
“Chini ya taratibu na Katiba, viongozi wa juu wamefanya uteuzi kwa wagombea ngazi ya mkoa ikiwamo mkoa wetu wa Dodoma. Rai yangu kwenu mtakapokuwa mnatekeleza jukumu hili la uchaguzi lazima mkumbuke mnao wajibu wa kutii uamuzi wa mamlaka za juu katika uteuzi waliofanya,” alisema.
Alisema fursa yao ni kukamilisha kwa kidemokrasia kwa kuchagua viongozi bora ambao watafaa kwa mkoa wa Dodoma.
“Mamlaka za juu zimewapa majina baada ya kuyachuja na wakaona wote wana sifa sahihi tuwapeleke sasa wakaamuliwe na wahusika wenyewe ambao ndio nyie mtasema huyu ndiye huyu,” alisema.
Aliwataka kutumia haki hiyo vizuri kwa kuwa ni msingi kwa kuchagua kiongozi bora asiye na makundi na ambaye atakuwa hajatoa rushwa.
“Hata kama ni rafiki yako hafai, jisikie huru kukataa kumchagua. Chagua kiongozi bora na awe na uwezo wa kuongoza ambaye hatakubaliana na fikra za kipuuzi,” alisema.
Aliwaasa kutokubali kuyumbishwa kwa vitendo vya rushwa kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwafanya kuchagua kiongozi ambaye hafai kuwa kiongozi bali ni fedha zake zimemweka katika uongozi