Government Jobs, Jobs in Dar es salaam, Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, Job listing website, It job finder, Search for jobs in my area, Job posting website, Job position, job listings, job postings, nursing employment, resume, post a job indeed, job search board, indeed cv database, post job
KULIWAANA
Kwasi ambaye ametua Lipuli akitokea Mbao FC ya Mwanza, alionyesha uwezo mzuri na kufanikiwa kuisawazishia timu yake bao katika mechi iliyopigwa Jumapili dhidi ya vinara hao wa Ligi Kuu, Simba wanaodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa.
Matola aliliambia gazeti hili jana kuwa, hata kama Simba itafanikiwa kumchukua beki huyo, kikosi chake hakitakuwa na pengo kwa sababu wapo mabeki wengine ambao wanauwezo na uzoefu wa kukabiliana na ushindani wa mechi za Ligi Kuu.
"Kama kweli Simba wanania ya kumsajili beki wetu, waje rasmi, na akiondoka sitakuwa na pengo kubwa kwa sababu tunaye Lufunga (Novalty) na Martine (Kazila) ambao ni wazuri na walishafanya vyema wakati Asante Kwasi akiwa majeruhi na alikosa mechi kadhaa za awali," alisema Matola.
Kiungo na nahodha huyo wa zamani wa Simba alisema pia katika dirisha dogo anahitaji kuboresha kikosi chake katika safu ya ushambuliaji na tayari ameshawasilisha barua kwa Wekundu wa Msimbazi akiwahitaji Juma Luizio na Jamal Mnyate.
Kwasi ana mkataba wa mwaka mmoja na Lipuli utakaomalizika mwakani na tayari ameshaanza mazungumzo ya chini kwa chini na Simba kwa ajili ya kujiunga nayo kwenye kipindi cha dirisha dogo.
Lipuli FC, Njombe Mji FC na Singida United ambayo iko katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ndio timu tatu zilizopanda daraja msimu huu. Government Jobs, Jobs in Dar es salaam, Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, Search for jobs in my area, Job posting website, job postings, nursing employment, job search board, indeed cv database, post job
 
Top