Tanzania, Government Job, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area
HATIMA ya Dk. Louis Shika aliyejizolea umaarufu kwa kauli ya "900 itapendeza" sasa iko mikononi mwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), imeelezwa.
Dk. Shika aliukwaa umaarufu huo alipotaka kununua nyumba tatu za kifahari za Kampuni ya Lugumi Enteprises kwa thamani ya Sh. bilioni 3.3 Novemba 9, mwaka huu, lakini asimudu kutoa asilimia 25 ya kiasi hicho siku hiyo kama kanuni za minada zinavyotaka.
Mnada huo ulioendeshwa na kampuni ya udalali ya Yono ulihusisha nyumba moja iliyoko Mtaa wa Mazengo, Upanga katika Manispaa ya Ilala na mbili zilizoko jirani na Kambi ya Mbweni JKT, Manispaa ya Kinondoni.
Chanzo chetu juzi kilizungumza na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, kutaka kujua hatima ya Dk. Shika baada ya kumuachia kwa dhamana ya kujidhamini mwenyewe katikati ya mwezi uliopita, lakini alisema jalada lake liko kwa DPP.
"Ukiona kesi haijafikishwa mahakamani ujue haina maslahi kwa umma, na unajua wakati wa mnada wa nyumba zile hapakuwa na madhara yaliyotokea na kwa sababu nyumba za Lugumi zipo na hazijatapeliwa, ule ulikuwa kama mchezo wa kushinda tu," alisema Mambosasa.
Aidha, Kamanda Mambosasa alisema kutokana na udogo wa kosa lenyewe ndiyo sababu aliamua Dk. Shika ajidhamini mwenyewe baada ya kukaa rumande kwa siku sita na kukosa mtu wa kumdhamini.
"Kwa hiyo kosa ni dogo, lakini tukipata jalada la kesi kutoka kwa DPP basi atafikishwa mahakamani. Mkiona kimya jalada halijatoka maana yake hakuna kosa hivyo hakutakuwa na kesi."
Novemba 9, Dk. Shika alikuwa miongoni mwa washiriki kwenye mnada wa kununua nyumba za Lugumi zilizokuwa zikipigwa mnada na Kampuni ya udalali ya Yono, lakini aliposhindwa kutoa asilimia 25 ya malipo kama masharti ya mnada yanavyotaka na badala yake kudai fedha zake zipo nje ya nchi, ndipo polisi ilipomkamata.
Chanzo: Nipashe
Tanzania, Government Job, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job