Tanzania Job, Government Job, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job 
Zaidi ya wahitimu 100 wa kozi ya Afya ya Jamii katika Chuo cha Sayansi ya Afya cha St. Agrey jijini Mbeya, wanakusudia kukifungulia mashtaka chuo hicho kwa madai ya kupoteza vyeti vyao vya kidato cha nne
Rais mstaafu wa Serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Noel Mng’ong’o, anasema wakati wanajiunga na chuo hicho Novemba 2015, waliambiwa wapeleke vyeti vyao halisi ili vipelekwe Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya uhakiki.
Anasema vilikusanywa vyeti vya wanafunzi wa kozi zote na vingine vilirejeshwa baada ya uhakiki isipokuwa vya wanafunzi wa kozi ya afya ya jamii ambayo tangu wakati huo wamekuwa wakifuatilia bila mafanikio.
Mng’ong’o anasema awali walikuwa na matumaini kuwa vyeti vyao vingepatikana, lakini matumaini hayo yalianza kufifia wakati wanakaribia kumaliza masomo kwa madai kuna mmoja wa watumishi wa chuo hicho aliwadokeza kuwa vyeti vyao havijulikani vilipo.
Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Rex Mwakipiti, anakiri kukusanya vyeti vya wanafunzi hao, lakini alisema ni vyeti vya wanafunzi 102 na siyo 111 kama inavyodaiwa. Tanzania Job, Government Job, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
 
Top