Lionel Mess,Jobs o, nursing jobs, Lionel Mess It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, Lionel Mess
Lionel Messi ametaja timu nne anazoamini zitaipa wakati mgumu Barcelona katika mbio za kusaka ubingwa wa Ligi ya Mabingwa, lakini hakumtaka Jose Mourinho na Manchester United yake wala Juventus.
Baada ya kuanza kwa kishindo msimu huu wa La Liga umemfanya Messi kuamini kiwango cha sasa ha Barcelona kinastahili kuwa moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo wa Ulaya.
Lakini Messi amewatadhalisha wachezaji zake wa Barcelona kuwa watapata wakati mgumu kutimiza ndoto yao ya kutwaa taji la sita la Ulaya kutoka kwa Manchester City, Paris Saint- German, Bayern Munich pamoja na mabingwa watetezi Real Madrid.
'[Man] City ni moja ya timu bora msimu huu pamoja na PSG,' alisema nyota huyo wa Argentina.
Lakini msimu ndiyo kwanza umeanza; Siwezi kuwaondoa Real Madrid kwa sababu ya ubora wa kikosi chake, japokuwa kwa sasa wanapata matokeo ya kubahatisha.
'Usiwasahau Bayern Munich - Bayern ni timu kubwa inaweza kukushangaza mwisho wa msimu huu.'
Wakati ikiwa imebaki mechi moja kabla ya kumalizika kwa mechi za makundi, ila klabu zote alizozitaja Messi tayari zimeshafuzu kwa hatua ya mtoano.
Wakati washindi wa pili msimu uliopita Juventus ipo katika hatari ya kuangukia Europa Ligi.
Manchester United pia haina uhakika kama itafuzu japokuwa vijana wa Mourinho wanatakiwa kufunga mabao sita katika mchezo wa mwisho dhidi ya CSKA Moscow ili ikose nafasi ya kucheza hatua inayofuata.
Lionel Mess,Jobs o, nursing jobs, Lionel Mess It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, Lionel Mess
 
Top