Jobs o, nursing jobs, It job finder, Search for jobs in my area, job postings, nursing employment, post job
Akizungumza kwa mara ya kwanza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, baada ya kuruhusiwa, Prisca, ambaye ni mwalimu mkoani Morogoro, alisema alipata tatizo la figo zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Alisema kutokana na tatizo hilo, alikuwa akifanyiwa usafishaji damu kwenye figo (dialysis) kila baada ya muda.
Prisca ambaye alimshukuru kaka yake, Bathromeo Mwingira (27), ambaye amemtolea figo, alisema Watanzania wengine wenye tatizo kama alilokuwa nalo wanaweza kuwatolea figo wenzao ili kuokoa maisha yao.
“Nina mshukuru Mungu kwa kufanyiwa upasuaji huu, pili ndugu yangu na madaktari waliofanikisha upasuaji wangu.
Sasa ninaweza kufanya shughuli zangu kama kawaida,” alisema Prisca huku akitokwa na machozi na kumkumbatia kaka yake.
Prisca ni mtoto wa sita kati ya watoto tisa wa familia ya Mwingira na Batholomeo ni mtoto wa saba.

UPASUAJI SAA NNE
Mtaalamu Bingwa wa Upasuaji na Magonjwa ya Figo, Dk. Jacqueline Shoo, alisema upasuaji huo uliofanyika Novemba 21, mwaka huu, ulichukua saa nne ili kupandikiza figo kwa Prisca.
Alisema upasuaji huo ambao ni wa kwanza nchini, umefanikiwa na baada ya siku 10 wamemruhusu Prisca kutoka hospitalini na kwenda kufanya shughuli zake za kawaida, baada ya madaktari kujiridhisha.
“Pamoja na kuwa ndani ya miezi sita atahitaji kutofanya kazi ngumu, pia aliyemtolea figo hataweza kufanya kazi ngumu katika kipindi hicho. Wanarudi nyumbani na kuishi mazingira ya kawaida kabisa na hawana tatizo lolote,” alisema Dk. Shoo.
Alisema kwa sasa Prisca ataendelea kutumia dawa, kuzingatia usafi, aina ya chakula kulingana na ushauri wa madaktari.

BABA MDOGO
Baba mdogo wa Prisca, Einhard Mwingira alisema anaishukuru serikali kwa kumgharamia mtoto wake (Prisca) matibabu hayo huku akiiomba serikali kumpatia uhamisho wa kikazi.
Alisema kutokana na kazi ya ualimu kuhitaji kutumia chaki anapofundisha ubaoni akiwa darasani, vumbi la chaki linaweza kumwathiri.
“Naiomba serikali impatie uhamisho kutoka Morogoro na kuhamia Dar es Salaam na hata matumizi ya chaki wakati wa ufundishaji yaangaliwe ili vumbi lake lisimdhuru,” alisema Mwingira.

GHARAMA UPASUAJI
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaesha, alisema matibabu hayo yaliyofanyika hapa nchini, yamegharimu Sh. milioni 21 na kwamba yangefanyika nje ya nchi, gharama yake ingekuwa Sh. milioni 80 hadi 100.
Alisema mafanikio hayo yamefikiwa baada ya madaktari bingwa wa MNH kwenda nchini India kwa ajili ya kupatiwa mafunzo zaidi kuhusu magonjwa ya figo.
Chanzo: Nipashe
Jobs o, nursing jobs, It job finder, Search for jobs in my area, job postings, nursing employment, post job
 
Top