Government Jobs, Employment Online,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
Jambo la kuzingatia ni kuwa hauwezi kufanikiwa kama utashindwa kujitofautisha na wengine kwa kuthibitisha kuwa wewe ni bora zaidi ya wengine utakaoshindana nao.
Siri kubwa ya kufanikiwa katika hili huwa ni maandalizi. Bila kujali una uwezo, uzoefu na ufauluwa kiasi gani, maandilizi ni jambo la msingi -- ushindi ni kwa wale waliojiandaa vyema.
LENGO LA USAILI NI NINI? Kabla ya kwenda kwenye usaili unatakiwa ujue shughuli hiyo ina lengo gani.
Najua wengi hudhani usaili ni kwa ajili tu ya kupima uwezo wako na kuona kama unafaa kwa ajili ya ajira. Ni kweli, lakini hilo siyo lengo pekee la shughuli hii. Usaili hutumiwa pia na mtafuta ajira ili kupima kama kazi anayotarajia kupewa inamfaa au inaendana na malengo yake.
Hii pia ni sehemu ya majadiliano na makubaliano yenye lengo la kufikia mwafaka wa mambo kadhaa kama malipo, kituo cha kazi na manufaa mengine baina yako na mwajiri. Usaili pia ni sehemu ya kufahamiana na kuifahamu taasisi vyema.
Kuliendea jambo hili, kuna mambo kadhaa ya msingi ambayo unatakiwa kufanya kama sehemu ya maandalizi ya usaili. Ukifanikiwa kuyafanya mambo hayo itakusaidia kukupa ujasiri na kukuongezea nafasi ya kufanya vyema katika usaili:
1. TAFUTA TAARIFA ZA TAASISI HUSIKA Kitu unachokipenda ni lazima ukifuatilie na unapokwenda kwenye usaili ni uthibitisho kuwa taasisi husika umeipenda. Huwezi kukipenda kitu usichokifahamu, hivyo ni vyema kutafuta taarifa zinazohusu taasisihiyo.
Hii itakufanya uwe tayari kuulizwa maswali yatakayoonyesha ni kwa kiasi gani unaifahamu au kuipenda taasisi husika.
Mambo ya msingi ya kufahamu juu ya taasisi ni pamoja na maono, dira, na malengo ya taasisi husika. Mambo mengine ni kuhusiana na huduma au bidhaa zinazotolewa na taasisi hiyo na aina ya wateja wanaowahudumia.
Majina ya viongozi na waasisi wa taasisi pia ni vyema uyafahamu kama inawezekana.
Swali uwa ni wapi unaweza kupata taarifa hizi zote? Taarifa hizi zinapatikana katika tovuti ya taasisi, mtandaoni, kupitia machapisho mbalimbali na wakati mwingine kupitia wafanyakazi wanaofanya kazi na taasisi hiyo.
2. JISOMEE MAMBO YAHUSUYO TAALUMA YAKO Maswali mengi katika usaili wa kazi huulizwa juu ya taaluma yako. Kama wewe ni mhasibu, waajiri huuliza maswali kuhusiana na uhasibu ili kujua ni kwa kiasi gani unafahamu kile utakachokua unakifanya.
Changamoto kwa wengi huwa ni namna ya kujisomea. Je, nisome kila kitu? Jibu ni hapana. Soma mambo ya msingi yahusuyo taaluma yako kwa sababu hautaulizwa kila kitu na hauwezi kujua kila kitu.
Pamoja na maandalizi ya taaluma yako, pitia kwa uchache mambo ya taaluma nyingine ambayo unahisi yatakuwa msaada katika ufanisi wa kazi yako.
3. REJEA BARUA YA MAOMBI NA CV Endapo ulituma wasifu (CV) na barua ya maombi ni vyema kupitia ili kujua ni nini ulikiandika. Maswali mengi pia huanzia kwenye barua na wasifu wako. Kama uliandika kuwa wewe ni mbunifu kuna uwezekano mkubwa waajiri wakataka uwathibitishie hilo.
Kupitia barua na wasifu wako, kutakusaidia kujiandaa kukabiliana na maswali yahusuyo taarifa ulizozitoa katika nyaraka hizo.
4. JIANDAE KWA MAJIBU YA MASWALI Jambo unalopaswa kufahamu ni ukweli kwamba asilimia kubwa ya maswali utakayoulizwa huwa yanafahamika.
Maswali kama jitambulishe; kwa nini tukuajiri wewe na si wengine; ungependa ulipwe mshahara kiasi gani; ni mojawapo ya maswali ambayo huwa yanaulizwa karibu katika kila usaili. Ni vyema kuyajua na kuandaa majibu yake mapema ili kujiongezea kujiamini. Kumbuka pia hauwezi kuandaa majibu ya maswali yote kwa sababu yapo mapya utakayoulizwa
5. FANYA MAZOEZI YA KUJIBU MASWALI Wengi hawapendi kukubali ukweli kwamba usaili kwa upande wa msailiwa una kiwango kikubwa sana cha sanaa. Na sanaa inahitaji ujuzi na uzoefu. Unapoenda kwenye usaili chukulia kama ni msanii anaenda kufanya onyesho kubwa. Katika mazingira haya bila shaka utajiandaa vyema kwa kufanya mazoezi mara kwa mara juu ya kile utakachokionyesha. Hivyo ndivyo huwa kwa usaili wa kazi.
Kwa mfano, binafsi, wakati naenda kwenye usaili wangu wa kwanza niliandaa maswali, nikaandaa majibu kisha nikafanya mazoezi mara kadhaa ya namna gani ya kuyajibu. Baada ya kuona niko tayari, niliwaita marafiki zangu, nikawapa maswali yale waniulize na mimi niyajibu; yaani kama tupo kwenye usaili wenyewe vile.
Baada ya kujibu niliwaomba wanikosoe. Wapo waliosema: “Kelvin unaongea kwa haraka sana.” Wengine wakasema: “Sauti yako haisikiki vizuri.”.
Na wengine wakaongeza: “Uko serious sana, hebu legeza uso kidogo.” Mawazo yao niliyafanyia kazi, kisha nikawaita tena waniambie kama nimejirekebisha.
Baada ya kupata mrejesho chanya nikasema sasa nipo tayari kwenda kwenye usaili. Hii ilinipunguzia uoga. Usaili wenyewe kwangu ulikuwa wa kwanza lakini ni kama nilikuwa nimeshakuwa mzoefu tayari kwa mazoezi niliyoyafanya.
6. JIANDAE KWA MAVAZI, NYARAKA Muonekano wako una nafasi kubwa sana katika kushawishi watu, hivyo kuwa makini na uchaguzi wako wa mavazi. Hakikisha haupanii maana usaili siyo onyesho la mziki wa dansi. Andaa mavazi yanayoendana na tamaduni za taasisi husika na hakikisha siyo mavazi yenye rangi zinazoumiza macho.
Jitathimini jinsi ulivonyoa au kusuka ili usionekane muhuni. Manukato yako yasiwe ya kukera wengine, yaani kwamba ile unaingia tu watu wanaanza kupiga chafya. Hakikisha chochote unachovaa hakikuhusishi na dini, dhehebu, chama cha siasa, timu ya mpira au chochote kinachoweza kukufanya ubaguliwe.
Kumbuka kuweka tayari nyaraka zote zinazohitajika kama vyeti vya elimu, kuzaliwa, na vyote vilivyoainishwa na mwajiri na ukumbuke kuvibeba.
Wiki ijayo tutaangalia mbinu na ujuzi katika kujibu maswali ya usaili

MATANGAZO YA AJIRA BOFYA HAPA  Employment Online,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
 
Top