Tangazo la Ajira,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
SIKU moja baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, kusema kuwa serikali haijakataza mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu za soka nchini, viongozi wa Klabu ya Simba wameanza mazungumzo ili kuruhusu mwekezaji kupewa asilimia 51, imeelezwa.
Waziri Mwakyembe ambaye kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa wanawachama wa Simba alisema juzi katika mahojiano na kituo kimoja cha radio nchini kuwa mchakato huo ni ruksa kuendelea lakini wawekezaji wanatakiwa kupewa hisa zisizozidi asilimia 49.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yamekamilika na wanawaomba wanachama kufika kwa wingi ili kufanya uamuzi wa pamoja wa aina ya mfumo utakaotumika kuingoza klabu yao.
Manara alisema kuwa wanaamini mazungumzo ambayo yanafanyika kati ya viongozi na klabu yatafikiwa muafaka na hatimaye kutangazwa kwa maombi ya mzabuni aliyeshinda.
"Tunatarajia mkutano huo utaandika historia ya mpira wa miguu katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, na katika kuhakikisha hili linafanyika kwa uwazi, Simba imewaalika viongozi mbalimbali kutoka TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), Bodi ya Ligi na wadhamini wa klabu yetu," alisema Manara.
Aliongeza kuwa wanatarajia Waziri Mwakyembe atakuwa mgeni rasmi katika mkutano huo endapo ratiba yake itamruhusu ili kushuhudia mapinduzi hayo yatakayofanyika ambayo yanalenga kuifanya klabu iweze kujiendesha kisasa.
Awali kabla ya kauli ya Waziri Mwakyembe kutoka juzi, ilitarajiwa mshindi wa zabuni atakayetangazwa katika mkutano huo wa kesho ni yule ambaye atakuwa tayari kutoa kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 20 kwa kupewa hisa asilimia 51.
Mchakato wa kubadilisha mfumo wa uendeshaji ndani ya Simba ulianza baada ya mfanyabiashara maarufu na mdhamini wa zamani wa klabu hiyo, Mohammed Dewji "Mo" kusema yuko tayari kutoka kiasi cha Sh. bilioni 20 na masharti ya kupewa asilimia 51 za hisa.
Baada ya mchakato huo kuanza, mmoja wa wanachama wa Yanga naye aliibuka na kusema yuko tayari kuikodisha klabu hiyo kwa muda wa miaka 10 kwa kupewa haki ya kumiliki asilimia 75 na kiasi kilichobakia ndio kitamilikiwa na wanachama
Chanzo: Nipashe
Tangazo la Kazi,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job