Government Jobs,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
TAARIFA na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii asubuhi hii zinaeleza kuwa gari dogo aina ya Toyota Land Cruiser (Prado) linadaiwa kuseleleka kutoka kwenye pantoni (Ferry) na kuzama baharini eneo la Posta jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi, Desemba 1, 2017.

Inadaiwa kwamba katika gari hilo binafsi kulikuwa na watu wanne ambao wote walizama nalo na mpaka tunaenda mitamboni ilikuwa haijajulikana kama wamenusurika au wamekufa.

Video hiyo inaonesha watu wakishangaa eneo la tukio huku mmoja wao akijitolea kwenda kulifunga kamba gari hilo ili livutwe na kuokolewa lakini kabla ya kulifikia, lilizama baharini na kupotea.

Chanzo chetu kimemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Emmanuel Lukula kuzungumzia tukio hilo ambapo amesema hana taarifa kwa kuwa alikuwa kwenye kikao hivyo anakwenda kufuatilia na atatoa ufafanuzi kuhusu tukio iwapo limetokea.

UKWELI NI HUU HAPA
Baada ya taarifa hizo kuendelea kusambaa, Chanzo chetu kimefuatilia zaidi na kubaini kuwa ukweli wa tukio hilo kuwa, gari hilo lilitumbukia jana Bahari ya Hindi nchini Kenya na si Dar es Salaam, Tanzania.

Daily Nation ya Kenya kupitia ukurasa wake wa Facebook waliripoti hilo jana hiyo hiyo na kufanya mahojiano na mmiliki wa gari lililozama na haya hapa ni mahojiano yake.

Chanzo: Global Publishers

Tangazo la Kazi,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
 
Top