Tangazo la Kazi,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
Akizungumza na chanzo chetu, mama mzazi wa binti huyo, Sakina, alidai kuwa alianza kusikia fununu juu ya uhusiano kati ya bintiye Mwanaisha na mumewe tangu mwanzoni mwa mwaka huu.
“Nilisafiri kwenda Tanga, niliporudi ndipo nikaanza kusikia fununu kwa majirani kwamba mwanangu ana uhusiano na mume wangu,” alidai mama huyo.
Alidai alipojaribu kuhoji aliishia kupigwa mateke na mumewe huku akimwambia asisikilize maneno ya uongo kutoka kwa watu wenye chuki naye.
“Kiukweli moyo wangu uliniuma sana baada ya kupata taarifa hizi za mwanangu kutembea na mume wangu niliyezaa naye watoto sita.
“Roho iliniuma kama mzazi lakini pia kwetu huu ni mkosi mkubwa mno kwenye familia. Baada ya kufahamu niliamua kumhoji mtoto lakini hakuweza kunieleza lolote lile, nilipomhoji mume wangu yeye aliishia kunipiga mabuti tena mbele za watu,” alidai Sakina.
Huku akifuta machozi, mzazi huyo aliendelea kusimulia kuwa, wakati huo tukio hilo linatokea, walikuwa wakiishi Kigogo Ruanga na baada ya suala hilo kuwa zito kwenye familia mumewe alimtimua pamoja na wanaye na akakimbilia maeneo ya Mabibo kujihifadhi kwa rafiki yake.
“Roho inaniuma sana, kwangu huu ni unyama wa kutisha na dira ya maisha yangu yote imeharibika. Mbali na hilo mwanaume huyu ameamua kunivua nguo na kunifedhehesha,” aliendelea kusimulia mama huyo.
Kwa upande wake Mwanaisha mwenye umri wa miaka 19, akizungumza na Amani namna alivyoanza kushiriki tendo la ndoa alisema hivi;
“Mimi baba alinibaka. Nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa kwanza siku moja asubuhi baada ya mama kuondoka kwenda kwenye biashara zake aliingia chumbani na kisu.
“Alianza kunilazimisha kufanya naye mapenzi huku akinitishia kwamba endapo sitakubali kile anachokitaka basi atanichinja.
Tangazo la Kazi,Jobs o, nursing jobs, Job listings inmy area, It job finder, Search for jobs in my area job postings, nursing employment, post job
 
Top